al-Bukhaariy amepokea kupita kwa al-Barraa´ aliyesema:

“Wakati Ibraahiym alipokufa – yaani mtoto wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema: “Yuko na mama wa kumnyonyesha Peponi.” Katika baadhi ya matamshi imekuja:

“Mwangu amekufa alipokuwa ananyonya. Ana mama wa kunyonya Peponi.”

Ikiwa haya ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi hakuna la kusema. Asli ni kutokuwa umaalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka pawepo dalili zenye kuonyesha kinyume, jambo ambalo hatuna hapa.

Ikiwa haya yanawahusu watoto wa waumini wote, kama ilivyokuja katika baadhi ya mapokezi ambayo siyakumbuki kwa hivi sasa, lakini maandiko yako kama ifuatavyo “Peponi kuna mti uliyo na matiti ambao watoto wananyonya kwenye mti huo”, basi ni bishara kubwa na liwazo kwa waumini juu ya watoto wao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 102
  • Imechapishwa: 17/10/2016