Kumzawadia mzazi asiye msomi thawabu za swalah na kisomo cha Qur-aan


Swali: Mama yangu mimi sio msomi na hajui kusoma wala kuandika. Je, inafaa kwangu kusoma Qur-aan tukufu na kuswali swalah za sunnah na kumzawadia thawabu zake? Ni mambo gani ninayoweza kumzawadia thawabu zake ikiwa haijuzu?

Jibu: Hakuna dalili inayokubalika katika Shari´ah juu ya kumzawadia mwengine swalah na kisomo cha Qur-aan. Ni mamoja mtu huyo yuhai au ameshakufa. ´Ibaadah ni kwa kukomeka; hakuna kinachokubalika katika Shari´ah isipokuwa kile ambacho Shari´ah imefahamisha juu ya kusuniwa kwake. Lakini imesuniwa kwako kumwombea du´aa, kumtolea swadaqah, kumhijia na kumfanyia ´umrah akiwa ni mtumzima ambaye hawezi kuhiji wala kufanya ´umrah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/321)
  • Imechapishwa: 18/07/2021