Kumuua mwanamke anapozini kwa kuchelea aibu

Swali: Huku kwetu Misri msichana akizini basi familia yake wanamuua kwa kuchelea aibu. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi?

Jibu: Kitendo cha kumuua hakijuzu. Isipokuwa akiwa aliwahi kuolewa. Kwa msemo mwingine amezini baada ya kuingia ndani ya ndoa. Katika hali hii atapigwa mawe. Hivo ndivo ilivyothibiti Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ndivo ilivyo ndani ya Qur-aan kama ilivyobaki hukumu yake na likafutwa tamko lake mpaka siku ya Qiyaamah.

Ama ikiwa bado hajaolewa basi ni lazima kumsimamishia adhabu ya Kishari´ah ambayo ni kumpiga bakora miamoja na kumfukuza mbali na mji mwaka mmoja kamili. Hapo ni pale ambapo katika kufanya hivo kutakuwa hakuna madhara yoyote. Ikiwa katika kufanya hivo kuna madhara, fitina, balaa na shari basi abaki nyumbani kwa familia yake na asitoje nje mpaka mwaka ukamilike.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (06) http://binothaimeen.net/content/6686
  • Imechapishwa: 31/10/2020