Kumuona mwanamke ambaye mtu anataka kumchumbia kwa njia ya intaneti


Swali: Mwanaume huyu anataka kumchumbia mwanamke lakini ameshindwa kukutana nae kwa kuwa anaeshi katika mji mwingine. Je, Kishari´ah inatosheleza akamuona kupitia intaneti?

Jibu: Kwa nini asisafiri? Kufanya hivi kuna heshima kwa walii wa mwanamke. Asafiri na amchumbie kwa walii wake. Kisha amuone baada ya wote kukubaliana na kuridhiana kisha baada ya hapo wakubaliane mahari na kuwekeana masharti. Halafu baada ya hapo ndio amtazame Kishari´ah.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/2805
  • Imechapishwa: 20/09/2020