Kuolewa na familia inayosifika kwa uchawi

Swali: Dada kutoka Ufaransa anauliza. Je, inajuzu kwangu kukataa mwanaume ambaye anataka kunichumbia. Wanajulikana kwa uchawi kati ya familia hii na upetukaji wa mipaka katika kutumia mali hata kama mwanaume huyo atakuwa na Dini na tabia nzuri na ametimiza sharti zote?

Jibu: Ikiwa mambo ni kama ulivyosema, basi kukataa kwako itakuwa ni wajibu. Usikubali kuolewa na mmoja wao. Ni juu yako kuwa na subira na uamini kuwa Allaah (´Azza wa Jall) atakutatulia matatizo yako. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا

“Yule mwenye kumcha Allaah, basi Allaah humtengenezea njia ya kutokea.”

Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia mtoto wa ami yake ´Abdullaah Ibn ´Abbaas (Radhiya Alllaahu ´anhumaa) miongoni mwa wasia alizompa:

“Na jua kuwa nusura inakuwa pamoja na subira, faraja inakuwa pamoja na matatizo na hakika pamoja na uzito upo wepesi.”

Check Also

Kaoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab ambaye hataki kuingia katika Uislamu

Swali: Nimeoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab kabla ya kuwa na msimamo, na nimepewa fatwa na baadhi …