Swali: Je, inajuzu kumuomba Allaah (Ta´ala) kwa haki ya viumbe, kama kusema “Ee Allaah! Ninakuomba kwa haki ya khaliyli Wako Ibraahiym”?

Jibu: Hapana, haijuzu kuomba kwa haki ya yeyote. Huna mafungamano yoyote na haki za viumbe. Haki ya kiumbe ni yake yeye na sio ya kwako. Wewe muombe Allaah kwa matendo yako wewe. Tawasssul kwa matendo yako binafsi na usitawassul kwa matendo ya wengine au wema wa wengine. Hili halifai. Tawassul kwa Allaah kwa matendo yako mema. Kuhusu matendo ya wengine ni ya kwake binafsi. Allaah (Ta´ala) Amesema:

تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ

“Huo ni ummah kwa hakika umeshapita, utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mliyoyachuma.” (2:141)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-9.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020