Swali: Kuna mtoto wa mtu mmoja nimempa jina la “Twalha”. Jirani mmoja akanikataza na kusema “Jina hili ni lipya katika jamii”. Unasemaje kuhusu hili?

Jibu: Subhaana Allaah. Twalha bin ´Ubaydillaah ni mmoja katika [Maswahabah kumi] waliobashiriwa Pepo. Vipi mtu asijiite kwa jina lake!?

Mtu kama huyu wakuta hakatazi majina ya magharibi yaliyojaa kati ya Waislamu leo. Kwa nini asiyakataze haya na badala yake anakataza jina la Twalha?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-5-25.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014