Swali: Ni ipi hukumu ya kumpa mtoto jina la “Maaria”?

Jibu: Kuitwa jina la Maaria hakuna neno. Ni jina linaloruhusu. Asli katika majina yote ni jambo mubaahah (linaloruhusu), isipokuwa ikiwa ndani ya jina hilo kutakuwa na kujifananisha na makafiri katika majina ya makafiri au ikawa ndani yake kuna kuelekezewa uabudiwa kwa asiyekuwa Allaah, kama “´Abdul-Husayn”, “´Abdul-Masiyh”, “´Abdul-Ka´bah”….

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13537
  • Imechapishwa: 06/10/2020