Swali: Je, kumkataza mtawala wa Kiislamu mbele ya watu ni haramu kwa makubaliano ya wanazuoni wote au ni masuala ya uongozi hata kama kunapatikana maslahi katika kumkataza?

Jibu: Ibra siyo kupatikana rai tofauti. Ibra ni kutazama ni nani yuko katika haki. Tunamfuata mwenye yuko katika haki. Maadumu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatuamrisha kusikiliza na kuwatii watawala wa Kiislamu hata wakifanya jeuri na kudhulumu. Anatuamrisha kwa hilo. Kwa kuwa hili ni katika kupitisha dhara dogo. Kwa kuwa kufanya uasi kwa watawala kunapelekea katika madhara makubwa kuliko subira ya jeuri na dhuluma yao. Maadamu ni waislamu. Jambo ikiwa litapelekea katika madhara makubwa, halijuzu. Haijuzu kupitisha kitu ambacho kitapelekea katika madhara makubwa na natija ya kinyume. Haijuzu hili.

وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ

“Wala msijitupe kwa mikono yenu katika maangamizi.” (02:195)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.subulsalam.com/site/audios/alfozan/divers/130.Asalafiya7aqi qatoha-13-6-1433.mp3 Tarehe: 1433-06-13/2012-05-04
  • Imechapishwa: 09/04/2022