Kumjamii mke katika swawm ya Shawwaal na deni la Ramadhaan

Swali: Kuna mtu amemjamii mke wake katika moja ya michana ya siku sita [za Shawwaal]. Je, analazimika kutoa kafara?

Jibu: Hakuna kinachomlazimu. Kafara ni kitu maalum katika mchana wa Ramadhaan. Hata katika swawm ya kulipa Ramadhaan. Endapo analipa deni la Ramadhaan kisha akafanya jimaa ndani yake anapata dhambi na haimlazimu kutoa kafara. Mtu ambaye analipa deni la Ramadhaan haijuzu kwake kufungua ni mamoja iwe kwa jimaa au kwa kula. Akiiharibu pasi na udhuru basi anapata dhambi. Lakini hata hivyo haimlazimu kutoa kafara.

Kuhusu masiku ya funga iliyopendekezwa ya sita hukumu yake ni moja. Hapati dhambi. Akipenda kuilipa ni vizuri. Asipoilipa basi hukumu yake ni moja kwa sababu ni swawm iliyopendekezwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 02/10/2020