Swali: Bora ni mtu kuleta Adhkaar za baada ya swalah wakati mtu amekaa au anaweza vilevile kuzileta wakati mtu yuko anatoka msikitini?
Jibu: Bora ni mtu kuzileta ilihali amekaa mkao uleule aliyomalizia swalah, kama ilivyotajwa katika Hadiyth. Lakini akiwa na kazi au na haraka, hakuna neno akaleta Adhkaar na huku anatembea:
فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ
“Mtakapomaliza swalah, basi mdhukuruni Allaah msimamapo na mkaapo na mnapolala ubavuni mwenu.”[1]
[1] 04:103
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (11) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/14466
- Imechapishwa: 10/10/2017