Kukusanya kati ya mapenzi na chuki kwa muislamu  

Ikiwa sababu ya kuchukia ni kwa ajili ya Allaah ni sawa. Hili ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Hili ni jambo linalotakikana na la sawa.

Ikiwa inahusiana na muislamu asichukiwe kwa jumla. Kwa haki ya muislamu ikibidi kuchukiwa, achukiwe upande fulani pamoja na kupendwa upande mwingine. Anapendwa kutokana na imani alio nayo, Tawhiyd na ´ibaadah na wakati huohuo anachukiwa kutokana na madhambi na maasi yake.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 483
  • Imechapishwa: 10/05/2020