Swali: Je, inafaa kukataa kushika mimba kwa sababu ya kunyonyesha kwa sababu akishika mimba nyingine basi maziwa yatakatika?

Jibu: Hili ni jambo kati ya mume na mke. Akimridhisha mume na wakapatana kwamba asimjamii kwa kuchelea asije kushika mimba au akatumia vidonge vya kuzuia mimba ili asishike mimba kwa sababu maziwa yaweze kubaki anyonyeshe na kumlea mtoto hakuna neno. Kutumia vidonge vya kuzuia mimba kwa ajili ya manufaa ya mtoto au manufaa ya mama kwa sababu pengine kushika mimba ni jambo linalomdhuru au zikawepo sababu nyenginezo zinazoeleweka na zisizokuwa na madhara hakuna neno.

Ama kitendo cha yeye kukataa jimaa peke yake kunaweza kumdhuru [mume]. Kitendo hicho kinaweza kupelekea katika shari kubwa kwa wote wawili kwa sababu ya kujizuilia na jambo la jimaa. Pengine akamwacha, akatumbukia ndani ya machafu na mfano wa hayo. Lakini bora zaidi ni yeye amjamii na akutane naye. Atumie kitu kinachozuia ujauzito akiwa anachelea mimba juu ya yule mtoto walienae. Kuna uwezekano vilevile mtoto huyu akapewa maziwa wanayonyweshwa watoto wachanga wengine. Ni sawa vilevile kumwachisha mtoto ziwa ikiwa itapelekea kufanya hivo. Hakuna neno pia mume na mke wakikubaliana juu ya kumwachia mtoto ziwa na badala yake kumlea kwa kitu kingine kama kwa mfano maziwa ya unga na vyenginevyo. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ

”Mkitaka kutafuta wa kuwayonyesha watoto wenu, basi si dhambi juu yenu.”[1]

[1] 02:233

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3689/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D9%85%D9%84-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D8%AC%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%B6%D8%A7%D8%B9%D8%A9
  • Imechapishwa: 06/11/2020