837- Nimemsikia Ahmad akiulizwa juu ya mtu ambaye kucha lake limevunjika katika Ihraam. Akajibu:

“Alikate.”

838- Nimemsikia Ahmad akiulizwa juu ya mwanamme ambaye amesuguasugua ndevu zake ambapo unywele ukadondoka. Akajibu:

“Kama unywele huo ulikuwa tayari umekwishatoka, basi hakuna kinachomlazimu.”

839- Nimemsikia Ahmad akisema:

“Mwenye kutoa unywele wake basi atoe 1.5 kg ya chakula.”

Bi maana wakati wa Ihraam.

840- Nimemsikia Muhrim mmoja akiwa na nywele mpaka kwenye mabega akisema kumwambia Ahmad:

“Nywele zangu zinanikera. Nizinyoe?”

Akajibu:

“Ukizinyoa basi utoe kafara ya kondoo au kufunga siku tatu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (1/143)
  • Imechapishwa: 14/04/2021