Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa ndugu muheshimiwa X (Allaah amsalimishe).

Salaamun ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Wa ba´d:

Narejelea swali lako ulilowauliza baraza la kielimu linalotoa fatwa wa nambari 2191 tarehe 06/10/1407 ambapo umeuliza hukumu ya kujengea msikiti karibu na makaburi kwa ajili ya kuwanufaisha waliyomo ndani ya makaburi kwa kitendo hicho, hukumu ya kuswali ndani ya msikiti huu na hukumu ya kuswali ndani ya msikiti ulio na makaburi.

Napenda kukujuza kwamba haijuzu kujenga misikiti kwenye makaburi. Aidha haijuzu kujenga msikiti karibu na makaburi kwa ajili ya kuwanufaisha wafu kwa kujenga msikiti pambizoni mwao.

Lakini makaburi yakiwa nje ya msikiti na kumepambanuliwa kati ya makaburi na msikiti barabara au kitu kingine mfano wake na hakujenga msikiti kwa ajili ya makaburi hayo, basi hapana neno kuswali ndani yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/302)
  • Imechapishwa: 20/09/2021