Miongoni mwa mambo pia yaliyokemewa na maimamu wa Salaf ni mijadala, ubishi na mizozo katika mambo ya halali na ya haramu. Haikuwa ni mwenendo wa maimamu wa Uislamu. Yalizuka baada yao pindi wanachuoni wa ´Iraaq na wafuasi wa ash-Shaafi´iy na wafuasi wa Abu Haniyfah walipoanza kuzozana juu ya mambo yenye tofauti. Walitunga vitabu vinavyozungumzia mambo ya tofauti na wakaingia kwa kina katika tafiti na kubishana juu yake. Yote hayo ni mambo yaliyozuliwa yasiyokuwa na msingi wowote. Hiyo ikawa ndio elimu yao mpaka jambo hilo likawashughulisha kuiacha elimu yenye manufaa. Salaf walikaripia jambo hilo. Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna watu waliopotea baada ya uongofu isipokuwa ilikuwa ni kwa sababu ya kuanza kujadili.” Kisha akasoma Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ

”Hawakukupigia mfano huo isipokuwa tu kutaka ubishi. Bali wao ni watu makhasimu.” [1]

Baadhi ya Salaf wamesema:

“Allaah akimtakia mja kheri, basi humfungulia mlango wa matendo na humfungia mlango wa mjadala. Allaah akimtakia mja shari, basi humfungia mlango wa matendo na humfungilia mlango wa mjadala.

Maalik amesema:

“Nilikutana na watu wa mji huu na kuwaona kuwa wanachukia ukithirishaji huu ambao watu waliyomo hii leo.”

Akikusudia mambo ya mataga.

[1]43:58 at-Tirmidhiy (3253) na Ibn Maajah (48). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (141).

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 20/09/2021