Kuitoa swalah nje ya wakati wake

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuswali lakini anaichelewesha swalah kutoka wakati wake?

Jibu: Akikusudia kuchelewesha swalah kutoka wakati wake, bila ya kuwa na udhuru, haikubaliwi. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا

“Hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.” (04:103)

Bi maana imefaradhishwa katika nyakati maaluum.

Imekuja pia katika Hadiyth:

“Swali swalah kwa wakati wake.”

Ikiwa hana udhuru wenye kumfanya akaichelesha kutoka wakati wake, haikubaliwi. Huku ni kuipoteza swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15201
  • Imechapishwa: 28/06/2020