Kuigiza sauti za waadhini


Swali: Ni ipi hukumu ya kuigiza adhaana kama kwa mfano mtu kuigiza adhaana ya Makkah au al-Madiynah au baadhi ya misikiti?

Jibu: Uigizaji wa sampuli yote ni jambo lisilosifika. Kila mmoja atoe kwa sauti yake aliyopewa na Allaah. Ajitahidi kuipamba sauti yake na wala asimuige muadhini mwingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-10-10.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014