Kuhusu Mtume kufupisha swalah Tabuuk siku kumi na nne

Swali: Ni jibu lipi kwa wale wanaotumia dalili ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali kwa kujumuisha na kufupisha kwa muda wa siku kumi na nne Tabuuk?

Jibu: Hili tumeshalijibu na mmesikia jibu. Mtume hakunuia kukaa. Alikaa huku anawasubiria maadui na hajui itachukua muda kiasi gani. Wanachuoni wa Fiqh wanasema mtu akikaa muda ambao hajui haja yake itaisha lini, afupishe swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (72) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14085
  • Imechapishwa: 16/11/2014