Kuhama kutoka katika nchi ya Kiislamu


Swali: Sisi tunaishi katika nchi ya Kiislamu ambapo Sunnah inapigwa vita waziwazi, kama vile ndevu, mwanamke kuvaa Hijaab na mengineyo. Yule mwenye kushikamana na Sunnah anajiweka katika mahojiano ya hapa na hapa. Je, inajuzu kuhama kwenda katika nchi nyingine ya Kiislamu?

Jibu: Si kwamba inajuzu; ni wajibu kuhama. Ikiwa hawezi kudhihirisha dini yake, basi hapo itakuwa ni wajibu kwake kuhama ikiwa ana uwezo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (81) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-1-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 17/02/2018