Kugawa Qiyaam-ul-Layl mara mbili


Swali: Qiymaam-ul-Layl inajuzu kuigawa mara mbili, nikaswali mwanzoni mwa usiku na nikaswali tena mwishoni mwa usiku?

Jibu: Jambo zuri. Usiku wote ni wakati wa swalah, mwanzoni wake, mwishoni wake na katikati yake. Vilevile ukiijumuisha mwanzoni mwa usiku, mwishoni mwa usiku au ukaigawa baina ya mwanzoni mwa usiku na mwishoni mwa usiku, hakuna neno kwa hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/montqa--1431-03-06.mp3
  • Imechapishwa: 20/09/2020