Kufupisha kwa mwenye kuwatolea swadaqah waliochelewa

Swali: Kuna mtu aliswali Dhuhr na akamaliza. Baadaye akaingia mtu msikitini na akataka kumtolea swadaqah ambapo akaswali pamoja naye akiwa imamu. Baada ya kumaliza Rak´ah ya kwanza wakaingia kundi la watu na wakawa wengi ambapo imamu baada ya kumaliza kuswali Rak´ah mbili akatoa salamu hali ya kuwa ni swalah ya sunnah. Je, kitendo chake ni sahihi?

Jibu: Ni lazima kwake kuswali kikamilifu na kuendelea pamoja nao. Anatakiwa aswali Rak´ah nne na awatolee swadaqah. Anahesabika amerudi kuswali mkusanyiko.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 13/07/2019