Bora I´tikaaf Makkah au misikiti mingine?

Swali: Ni lipi bora kufanya I´tikaaf katika msikiti Mtakatifu au katika misikiti mingine pamoja na kubainisha sababu?

Jibu: Ni jambo linalotambulika kuwa kufanya I´tikaaf katika msikiti Mtakatifu ndio bora zaidi. Isipokuwa ikiwa kama mtu katika misikiti hiyo mingine anakuwa na unyenyekevu zaidi. Kwa sababu wapo watu ambao kutokana na ule wingi na msongamano wanakuwa hawana unyenyekevu. Katika hali hiyo tunamwambia afanye I´tikaaf katika misikiti mingine unapoweza kuwa na unyenyekevu zaidi. Ama mbali na Makkah, misikiti mingine mikubwa ambayo kunaswaliwa ijumaa ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (52) http://binothaimeen.net/content/1185
  • Imechapishwa: 13/07/2019