Kufanya uso kuwa mbaya


Swali: Ni ipi hukumu ya kukata ndevu kwa pembezoni, urefu wake, kidevu na shingoni?

Jibu: Ukikata pembezoni mwake na urefu wake unaziondosha zote. Ni kwa nini unataka kuzifanya vibaya ndevu zako au kuufanya vibaya uso wako? Ndevu ni uzuri wa mwanaume. Zinatofautisha kati ya mwanaume na mwanamke. Allaah amekuneemesha kwazo. Allaah amekupamba nazo. Usizifupishe huku na kule. Usizifanye vibaya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (58) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16539
  • Imechapishwa: 23/09/2017