Kufanya I´tikaaf kinyume na radhi za wazazi

Swali: Mfanya I´tikaaf akitoka kwenda kufanya I´tikaaf pasina radhi ya wazazi wawili. Je, I´tikaaf yake inakuwa sahihi?

Jibu: Ikiwa wazazi wake wanamuhitajia, kuwatendea wema ni wajibu na I´tikaaf ni Sunnah. Ama ikiwa hawamuhitajii na hawadhuriki kwa hilo, ni juu yake kufahamiana nao na kupata radhi zao na afanye I´tikaaf. Vovyote itavyokuwa kusiwe baina yao mvutano.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-14.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014