Kufa Makkah na Madiynah kunajulisha kheri?


Swali: Je, kufa ndani ya msikiti Mtakatifu kunajulisha kheri? Je, kuzikwa Makkah na Madiynah kuna ubora ukilinganisha na kwengine?

Jibu: Kumepokelewa juu ya hayo Hadiyth ambazo ni dhaifu. Kinachozingatiwa ni matendo. Yakiwa matendo ya mtu ni sahihi basi yuko katika kheri hata kama atakufa katika ardhi yoyote. Na yakiwa ni maovu basi hakumfai kitu kufa Makkah au Madiynah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 17/01/2021