Kuchelewesha siku sita za Shawwaal zikutane na masiku meupe na jumatatu na alkhamisi

Swali: Kuna watu ambao wanachelewesha swawm ya siku sita za Shawwaal mpaka katika masiku meupe, jumatatu au alkhamisi. Ni kipi bora; kufululiza au kuchelewesha?

Jibu: Kufululiza ndio bora. Kwa sababu siku hizi zinafuata baada ya Ramadhaan. Ni kama mfano wa Raatibah. Bora ni yeye pale tu anapoanza kufunga katika ile siku ya pili ya Shawwaal afululize. Hili halina shaka. Jengine ni kwamba akinuia haya masiku sita kwamba ni masiku meupe inatosha. Kwa sababu anazingatiwa kuwa amefunga siku tatu katika kila mwezi. Halafu jengine ni kwamba masiku haya – jumatatu na alkhamisi – yatampitikia. Ni lazima yampitikie. Hivyo atapata thawabu za yote hayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/946
  • Imechapishwa: 09/12/2018