Kuandikiana deni ni wajibu?

Swali: Maneno Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ

“Enyi mlioamini! Mtakapokopeshana deni kwa muda maalumu basi liandikeni.” (02:182)

Je, maamrisho ya kuandikiana deni ni ya wajibu? Anayemkopesa mtu na wasiandikiane deni hili wanapata madhambi?

Wanachuoni wanasema kuwa maamrisho haya ni ya maelekezo na sio ya wajibu. Kuandikiana imependekezwa na sio wajibu. Ni maamrisho ya maelekezo na sio ya ulazima na ya wajibu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-14.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020