Swali: Je, inajuzu kuandika chini ya Aayah kwenye msahafu kwa kalamu ya mkaa ili nisisahau?

Jibu: Haijuzu kamwe kuandika kwenye msahafu. Hakuandikwi kwenye msahafu baina ya Aayah wala pembezoni mwake. Ndani ya msahafu hakuandikwi chochote kabisa, hakubaki ndani yake isipokuwa Qur-aan tu. Unapotaka kuandika, tafuta kitabu au karatasi pembeni na uandike unachotaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/5428
  • Imechapishwa: 24/09/2020