Kimsingi damu imtokayo mwanamke huwa ni hedhi

Swali: Ikiwa mwanamke hawezi kupambanua damu yake, je, achukulie kuwa ni hedhi, istihaadah au kitu kingine? Je, mtu achukulie damu hii nini?

Jibu: Kimsingi damu inayomtoka mwanamke huwa ni hedhi mpaka pale ambapo itaonekana kuwa ni istihaadhah. Kwa ajili hiyo, achukulie damu kuwa ni hedhi mpaka pale ambapo itadhihiri kuwa ni istihaadhah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/275)
  • Imechapishwa: 24/09/2020