Mwanamke wa hedhi kuswali kwa ajili ya haya

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwanamke mwenye hedhi kuswali kwa sababu anaona aibu?

Jibu: Hakutawadha?

Swali: Anasimama ili aswali kwa kuwa anaona aibu ikija itajulikana ya kwamba yuko na hedhi.

Jibu: Swalah ni haramu kwake. Hatakiwi kuswali ikiwa yuko na hedhi au ametwaharika na hedhi yake kabla ya kuoga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (40 B)
  • Imechapishwa: 24/09/2020