Kila Mahali Hajaawirah Wanaingiza Mguu Ni Lazima Kutokee Fitina


Abu ´Amr ´Abdil-Kariym al-Hajuuriy alienda India na baadaye akarudi Yemen na kuwafanyia Tabdiy´ Mashaykh Salafiyyuun wa India. Shaykh Rabiy´ akajadiliana naye nyumbani kwake ya kwamba anawajua na anaijua Salafiyyah yao. Hili khaswa ukizingatia ya kwamba Shaykh Rabiy´ aliikaa India kwa muda ambao sio mdogo. Lakini hata hivyo ´Allaamah huyu Abu ´Amr al-Hajuuriy hakukinaika na hayo! Badala yake akaendelea kung´ang´ania na kufanya ukaidi. Hivyo ndivyo alivyonieleza ndugu yetu Shaykh Haaniy ambaye alikuwepo katika kikao hicho. Akatoka na hakubadili msimamo wake wa kuwafanyia Tabdiy´. Kwa kuwa maamrisho hayo hayakutoka kwa kiongozi wa waumini Yahyaa al-Hajuuriy. Maamrisho yake tu ndio yawezayo kubadili msimamo.

Kuna mfuasi mwengine wa al-Hajuuriy alienda UAE na akarudi huku kwetu Yemen na kuandika kitabu ambapo akitahadharisha juu ya Shaykh ´Abdul-Baariy.

Hii ndio hekima walionayo watu hawa. Haya ndio matunda yao. Hii ndio Da´wah yao ulimwenguni kote. Hakuna wanachofanya isipokuwa ni kuihujumu Da´wah ya Salafiyyah, kuwabughudhi Salafiyyuun na kutahadharisha walinganizi wake. Wamefanya hivo Indonesia, Tanzania, Mexico, Hispania, kusini kwa Marekani na sehemu zengine zote. Wanaenda kote huko kuiharibu Da´wah Salafiyyah na kuwatahadharisha walinganizi wake wakweli. Lengo wanataka watu wawe nyuma ya al-Hajuuriy peke yake pasi na wengine.

  • Mhusika: Shaykh Abu ´Ammaar ´Aliy al-Hudhayfiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://m-noor.com/showthread.php?p=33728
  • Imechapishwa: 19/02/2017