Swali: Je, Hadiyth hii kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) imesihi ya kwamba ikifika siku ya Qiyaamah ataita mwenye kuita upande wa Allaah (Ta´ala):

“Tanabahini! Hakika yule ambaye jina lake alikuwa akiitwa “Muhammad” asimame na kuingia Peponi” kwa ajili ya kumkirimu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Haya ni katika wanayoyapamba wao wenyewe. Sio Hadiyth. Kwa sababu tu mtu anaitwa Muhammad ndio aingie Peponi? Kuna makafiri ambao wanaitwa Muhammad. Je, na wao pia wataingia Peponi?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (63) http://alfawzan.af.org.sa/node/16495
  • Imechapishwa: 26/08/2017