Khawaarij hawatofautishi kati ya shirki na madhambi mengine

Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.” (an-Nisaa´ 04:48)

Ametofautisha (Ta´ala) kati ya shirki na madhambi mengine na akabainisha kuwa shirki haisamehewi na kwamba madhambi mengine yako chini ya matakwa Yake; akitaka kumuadibu basi atamuadhibu mwenye nayo, na akitaka kumsamehe basi atamsamehe mwenye nayo. Hata hivyo Aayah na Hadiyth ni lazima zifahamike juu ya mtu ambaye amekufa pasi na kutubu. Vinginevyo mwenye kutubu juu ya shirki anasamehewa. Asiyekuwa mshirikina ana haki zaidi ya kusamehewa.

Nilitumia dalili hizi dhidi ya kundi chipukizi waliozuka hii leo ambao wanakufurisha waislamu watenda madhambi makubwa, na wakati mwingine wanakata kabisa kwamba hawako chini ya matakwa ya Allaah na kwamba Aayah haiwahusu wale ambao hawakutubu. Hivyo wamelinganisha kati ya shirki na madhmbi makubwa na hivyo wakawa ni wenye kwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Wakati nilipotumia masaa na vikao vingi kwa watu hawa kwa ajili ya kuwasimamishia hoja, baadhi yao walijirejea katika usawa na wakawa Salafiyyuun wazuri. Allaah awaongoze wale wengine waliobaki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/3/1636)
  • Imechapishwa: 09/08/2020