Swali: Mimi nafanya kazi pamoja na wanawake. Ni ipi hukumu?

Jibu: Hili ni khatari. Kufanya kazi pamoja na wanawake ndani yake kuna khatari kubwa. Kwa sababu unakurubiana nao na unawatazama. Kuchanganyikana nao ni njia inayopelekea katika shari nyingi. Nasaha zangu kwake ajiepushe na kazi hii na badala yake afanye kazi katika maeneo ya wanamme na si maeneo ya wanawake. Kazi ziko nyingi. Yaliyoko kwa Allaah ndio bora na yenye kubaki. Aachane na kufanya kazi pamoja na wanawake na afanye kazi na wanamme badala ya jambo la wanawake. Wasimamizi wa wanawake wanatakiwa wawe wanawake wenziwe; daktari wa kike awe pamoja na madaktari wa kike wenzake, wauguzi wa kike wawe pamoja na wauguzi wa kike wenzake. Vivyo hivyo mwanamme kama ni daktari awe pamoja na wauguzi wa kiume wenzake na muuguzi wa kiume awe pamoja na wauguzi wa kiume wenzake. Akipupia na akamcha Allaah juu ya jambo hilo basi Allaah atamfanyia wepesi jambo lake. Lakini akichukulia wepesi na akayapa kipaumbele maisha ya dunia basi jambo hilo lina khatari kubwa ambayo inachelewa juu ya dini yake na juu ya tabia yake kutokana na kupotoka kwa sababu ya kuchukulia wepesi huku.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4630/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%85%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AE%D8%AA%D9%84%D8%B7-%D8%A8%D9%8A%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AC%D8%A7%D9%84-%D9%88%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%B3%D8%A7%D8%A1
  • Imechapishwa: 15/11/2020