Katika hali hii ni lazima kumtahadharisha kwa jina lake


Swali: Kuhusiana na mtu ambaye ametumbukia katika Bid´ah mbalimbali katika vitabu na maneno yake, je, ni sharti kumsimamishia hoja mtu huyu, au mtu mwengine, kabla ya kumwacha kama mzushi?

Jibu: Ikiwa mtu huyu anapatikana na watu wanachukua elimu kutoka kwake na analingania katika jambo hilo, basi ni lazima kumtaja jina lake. Vinginevyo hakuna haja. Taja maoni ambayo amepinda kwayo na ubainishe kuwa ni upotofu. Nilikwambia punde kidogo kwamba kutaja kosa ni bora kuliko kumlenga mtu. Lakini kama watu wanachukua Bid´ah zake, basi katika hali hii tunaweza kusema kwamba ni lazima kumtaja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (69 B)
  • Imechapishwa: 11/07/2021