Katika hali hii hapana neno kuingia chooni na Aayah za Qur-aan

Swali: Niliingia choo cha nyumbani kwangu hali ya kuwa na baadhi ya karatasi zilizo na utajo wa Allaah na Aayah za Qur-aan. Je, napata dhambi kwa hilo?

Jibu: Imechukizwa kuingia chooni na kitu kilicho na utajo wa Allaah. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alipokuwa anataka kuingia chooni basi huvua pete yake kwa sababu ilikuwa imeandikwa “Muhammad ni Mtume wa Allaah”.  Lakini kusipokuwa na wepesi kupata mahali salama ambapo anaweza kuweka karatasi mpaka pale atapotoka nje ya choo, basi katika hali hiyo hakuna neno kuingia nayo ndani. Kwa sababu ametenzwa nguvu kufanya hivo. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

“… na ilhali ameshakubainishieni yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo.”[1]

Kama Allaah ameruhusu kilicho haramu wakati wa dharurah basi kilichochukizwa kina haki zaidi ya kuruhusiwa.

[1] 06:119

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/30)
  • Imechapishwa: 31/07/2021