Swali: Huku Urusi watu hawavai kile kinachoitwa “thawb ya kisaudi” au “kanzu ya kiarabu”. Ni ipi hukumu ya kijana wa Kiislamu kuvaa hivo huku? Je, inazingatiwa kuwa ni kivazi cha kutaka kuonekana?

Jibu: Kinachotakikana ni yeye kufunika viungo vyake visivyotakiwa kuonekana. Anatakiwa kuvaa kama wanavyovaa watu wa mji wake isipokuwa ikiwa kama ni kivazi cha haramu. Katika hali hii asikivae. Ama ikiwa ni kivazi kinachoruhusiwa, naye atakiwa kuvaa hivo. Asijifanye maalum kwa kivazi ili isije kuwa ni kutaka kuonekana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (43) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2019%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020