Kafiri anataka kupewa msahafu


Swali: Mnaswara akiniomba Qur-aan nimpe au nisimpe?

Jibu: Usimpe. Lakini msomee, msikilizishe, mlinganie kwa Allaah na mwombee uongofu. Amesema (Ta´ala):

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ

“Endapo mmoja katika washirikina atakuomba umlinde, basi mlinde mpaka aweze kusikia maneno ya Allaah kisha mfikishe mahali pake pa amani.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msisafiri na msahafu katika ardhi ya adui isije kufika mikononi mwao.”

Hilo limefahamisha kwamba kafiri hapewi Qur-aan kwa kuchelea asije kuitweza au akacheza nayo. Lakini hata hivyo afunzwe, asomewe Qur-aan, aelekezwe na aombewe du´aa. Akisilimu ndio atapewa Qur-aan.

Lakini hapana neno akapewa baadhi ya vitabu vya tafsiri ya Qur-aan, baadhi ya vitabu vya Hadiyth akiona kuwa au baadhi ya tarjama za maana ya Qur-aan ikiwa kuna matarajio kuwa atanufaika kwayo.

[1] 09:06

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/444)
  • Imechapishwa: 26/02/2021