Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa ´Abaa´ah ya mapambo, anaweka ´Abaa´ah mabegani na kuvaa suruwali?
Jibu: Suruwali haijuzu kwa mwanamke. Suruwali sio vazi la mwanamke. Mwanamke anatakiwa kuvaa vazi pana, lenye kusitiri na lililo la wasaa. Haijuzu kwake kuvaa mavazi ya kubana. Suruwali ni vazi la kubana. Haijuzu kwake.
´Abaa´ah la mapambo halijuzu. ´Abaa´ah ni kwa ajili ya kujisitiri. Sio kwa ajili ya kujipamba. ´Abaa´ah halitakiwi kuwa na mapambo na michoro.
Wakati anapotoka ´Abaa´ah anatatakiwa kuliweka juu ya kichwa. Hata hivyo hakuna neno akaliweka mabegani mwake anapokuwa nyumbani au pamoja na wanawake wenzake.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Liqaa’-ul-Jumu´ah bit-Twaa’if http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17101
- Imechapishwa: 24/09/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Mwanamke anakata nywele zake na anavaa suruwali kwa ajili ya mume
Swali: Ni ipi hukumu juu ya kukata nywele na kuvaa suruwali kwa ajili ya mume? Jibu: Uzuri unapatikana katika nywele za mwanamke na sio katika kuzikata. Yeye kukata ina maana anajifananisha na wa magharibi na wanawake ambao hawajali uzuri wao. Nywele za mwanamke ndio mapambo yake na aziache kama zilivyo na…
In "Suruwali kwa mwanamke"
Mwanamke kuonesha mikono na sehemu katika nywele zake
Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuonesha sehemu katika nywele zake kwa kukusudia pamoja na kuvaa ´Abaa´ah na shungi? Je, kwa kufanya hivi anazingatiwa kuwa ni mwenye kufanya mapungufu katika Hijaab au ni mwenye kuonesha mapambo? Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kuonesha kitu katika nywele zake. Bila ya shaka huku ni kuonesha…
In "Jumla kuhusiana na vazi la mwanamke"
Jilbaab za mapambo na za marembo
Swali: Leo kumeenea ´Abaa´ah zilizopambwa kwa rangi mbalimbali. Ni ipi hukumu ya kuziuza na ni ipi hukumu ya kuzivaa? Jibu: Hizi sio ´Abaa´ah; hii ni mizigo (عبء). Haijuzu kuziuza wala kuzivaa. ´Abaa´ah zimewekwa kwa ajili ya kuficha mapambo. Hazikuwekwa kwa ajili ya kutaka watu wakuone. Wakati walipoona wanawake wa Kiislamu…
In "Jilbaab na ´Abaayah"