Swali: Je, roho zinakutana baada ya kufa?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kumekuja mitazamo mingi kuhusu kukutana na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi. Kumepokelewa mambo yanayojulisha kuwa zinaweza kukutana ambapo roho ya muumini inakutana na roho ya muumini ambaye bado yuko hai wanakutana usingizini. Kumepatikana mifano mingi inayojulisha kupatikana kwa jambo hilo. Lakini hakuna juu ya hilo Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inayofahamisha hilo kutokana na tunavyojua. Lakini kumepatikana ndoto zinazojulisha juu ya jambo hilo na juu ya kutokea kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/2988/%D9%87%D9%84-%D8%AA%D8%AA%D9%84%D8%A7%D9%82%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B1%D9%88%D8%A7%D8%AD-%D8%A8%D8%B9%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%88%D8%AA-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%A8%D9%88%D8%B1
  • Imechapishwa: 08/02/2020