Je, hii leo wako ambao wamebeba fikira za Khawaarij?


Swali 27: Je, hii leo wako ambao wamebeba fikira za Khawaarij?

Jibu: Kutakasika ni kwa Allaah kutokamana na mapungufu! Haya yanapatikana hii leo. Kuwakafirisha waislamu sio matendo ya Khawaarij? Baya zaidi kuliko hilo ni kuwaua waislamu na kuwashambulia kwa vilipuzi. Haya ndio madhehebu ya Khawaarij. Yamejengeka kutokamana na mambo matatu:

1- Kuwakufurisha waislamu.

2- Kujitoa nje ya utiifu wao.

3- Kuhalalisha damu ya waislamu.

Haya ndio madhehebu ya Khawaarij. Hata kama ataamini hivo ndani ya moyo wake na asizungumze na asifanye chochote anakuwa Khaarijiy katika imani yake na mtazamo wake iliyomganda.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 140
  • mkusanyaji: Abu Ashbaal Ahmad bin Saalim al-Miswriy