´Iyd-ul-Fitwr ni siku moja na ´Iyd-ul-Adhwhaa ni siku tatu

Ramadhaan ni mwezi mkubwa. Inafuatiwa na ´ibaadah na utiifu na si na mambo ya kipuuzi, michezo, maasi, maovu na mambo mbali mbali ya mapumbazo yanayofanywa na watu. Huenda wakafikia mpaka kufanya mchezo na Swalah kwa wakati wake. Hoja yao ni kwamba ni masiku ya ´Iyd. Pamoja na hivyo ni siku moja ya ´Iyd na sio masiku mengi. ´Iyd-ul-Adhwhaa ndio ina masiku mengi. ´Iyd-ul-Fitwr ina siku moja tu. Masiku yaliyo baada yake sio Idi. Lakini watu wameikuza mpaka wake, wanaita ´masiku ya Idi` na wanafanya mambo yasiyoridhia Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ili wafuatishe mwezi wa Ramadhaan kwa maasi. Hawauheshimu mwezi huu. Hii ni khasara na ni maangamivu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/%205843
  • Imechapishwa: 03/05/2015