ISIS, an-Nusra Na al-Ikhwaan al-Muslimuun hayajaupa Uislamu manufaa yoyote


Swali: Kuna watu wanaowahamasisha vijana wa Kiislamu na ´Awwaam kujiunga na mfumo wa kigeni na wa kikundi kama an-Nusrah, ISIS na al-Ikhwaan al-Muslimuun na kusema kuwa hii ndio njia sahihi?

Jibu: Ndugu! Makundi yote yaliyozushwa yaliyopo hii leo ni upotevu. Ukitazama kwa umakinifu basi utaona kuwa makundi haya hayakuupa Uislamu lolote na wamejivisha Uislamu katika maoni na matamanio yao ili kuwatia watu mchanga wa machoni. Vinginevyo ni upotevu. Wanaonelea kuwa ni halali kumwaga damu, kuvunja heshima za watu, kupora mali na uharibifu tele. Mifumo yote hii ni ya kipotevu. Allaah tu ndiye Ajuae aliyeko nyuma yayo. Hakuna kheri yoyote ndani yayo. Hatuwaamini wala wale wenye kuyafanya. Yule mwenye kuwahamasisha vijana katika mapote haya anafanya makosa na amepotea.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/QJdGgiBSDTI
  • Imechapishwa: 15/11/2014