Inasihi kula kichinjwa ambacho mchinjaji amesahau kusema Tasmiyah?


Swali: Nilisahau kutaja jina la Allaah wakati wa mawindo. Je, kiwindwa kinasihi?

Jibu: Kuna tofauti. Maoni ni ya sawa ni kwamba mtu akicha kutaja jina la Allaah wakati wa mawindo na wakati wa kuchinja kinasihi [kichinjwa]. Wapo wanachuoni wenye kuona kuwa hakisihi. Wengine wakasema kwamba kinaanguka ni mamoja iwe kwa kusahau au kwa kukusudia. Maoni ya kati na kati ni kwamba akisahau kinasihi. Ama akiacha kwa kukusudia hakisihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 15/09/2018