Inafaa kwa mwanaume kumuosha msichana na mwanamke kumuosha mvulana?

Swali: Inafaa kwa baba au mama kumuosha mtoto wao anayekufa aliye chini ya miaka saba?

Jibu: Baba anaweza kumuogesha msichana wake akifa na yuko chini ya miaka saba. Mama anaweza kumuogesha mvulana wake akifa na yuko chini ya miaka saba. Ibraahiym, mvulana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alipokufa alioshwa na mwanamke18. ´Awrah chini ya miaka saba haina hukumu yoyote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/85-86)
  • Imechapishwa: 06/09/2021