3161- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwache huru. Kwani hakika ni muumini.”

Ameipokea Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, ad-Daarimiy, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh”, al-Bayhaqiy katika ”as-Sunan”, Ahmad, al-Bazzaar katika ”al-Musnad” na at-Twabaraaniy kupiita Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Muhammad bin ´Amr, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka ash-Shariyd bin Suwayd ath-Thaqafiy.

Hakika Hadiyth ambayo ni Swahiyh zaidi katika hizo zilizotangulia ni Hadiyth ya Mu´aawiyah[1]. Kwa hivyo si ajabu kuona wanachuoni katika Muhaddithuun na Fuqahaa´ daima na siku zote wanakubaliana kuisahihisha. Hakuna tofauti yoyote kati yao. Imesahihishwa na wale watano ambao wana sharti ya kuzisahihisha Hadiyth Swahiyh peke yake. Vivyo hivyo al-Bayhaqiy ameisahihisha katika “al-Asmaa´ was-Swifaat”. Pia al-Baghawiy katika “Sharh-us-Sunnah”. Vilevile adh-Dhahabiy. Pia Ibn Hajar amefanya hivo katika “Fath-ul-Baariy”. Wote hawa wamesema waziwazi kwamba Hadiyth ni Swahiyh na cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Miongoni mwao wanaingia pia wale maimamu katika Hadiyth, Fiqh na wafasiri wa Qur-aan ambao wameijengea hoja, pamoja na kutofautiana kwa madhehebu yao. Baadhi yao ni Maalik katika ”al-Muwatta’”, ash-Shaafi´iy katika ”al-Umm”, Ahmad katika ”Masaa-il-ul-Imaam Ahmad” ya ´Abdullaah bin Ahmad na Swaalih bin Ahmad, at-Twahaawiy katika ”Sharh-ul-Ma´aaniy”, Ibn ´Abdil-Barr katika ”al-Istiy´aab”, Ibn-ul-Jawziy kaika ”Daf´ Shubah-it-Tashbiyh”, an-Nawawiy katika ”al-Majmuu´”, Ibn-ul-Waziyr katika ”al-´Awaaswim min al-Qawaaswim” na wengineo wengi.

Miongoni mwao wako mpaka baadhi ya watu wa Bid´ah ambao wanatambulika juu ya chuki yao dhidi ya Ahl-us-Sunnah, kama mfano wa Shaykh as-Swaabuuniy. Amekubaliana na Haafidhw Ibn Kathiyr ambaye amesahihisha Hadiyth hiyo na akaitaja sehemu mbili katika ufupisho wake ambapo amejichukulia sharti ya kutosahihisha isipokuwa tu zile Hadiyth ambazo ni Swahiyh.

Ama kuhusu watu wa Bid´ah waliopindukia na watu walioathirika na Jahmiyyah hii leo, baadhi yao wametangaza kwamba Hadiyth hii ni dhaifu. Wamepinga usahihi wa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema “Allaah yuko wapi?” na jawabu la kijakazi “Juu mbinguni.” Wanaoshika nafasi ya mbele kabisa katika watu hawa ni Shaykh al-Kawthariy na wale wanaomfuata kichwa mchunga. Nimemchapa Radd ipasavyo katika kitabu changu “Mukhtaswar-ul-´Uluww” na hakuna haja ya kukariri tena mahala hapa.

[1] Muslim (537), Abu Daawuud (930), an-Nasaa’iy (3/13), Maalik (2/776), Ibn Abiy ´Aaswim (479), al-Bayhaqiy, uk. 422, Ahmad (5/447), Abu Daawuud at-Twayaalisiy (1105) na Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 121.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/1/470-471)
  • Imechapishwa: 17/04/2020