Ikiwa kijana yuko na uwezo wa kuoa na aoe hata kama baba na mama yake

Ikiwa kijana yuko na uwezo wa kuoa na aoe hata kama baba na mama yake watamkatalia. Mbele yako uko na maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo yanatangulizwa kabla ya maamrisho ya wazazi wawili. Upande mwingine akiwa si muweza na hana pesa na wakati huo huo baba yako akawa na pesa,  ni wajibu kwa baba yako kukuozesha. Endapo atakataa anapata dhambi. Baba yako akiwa fakiri, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaelekeza vijana iwapo hawana uwezo wa kuoa wafunge. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Afunge, kwani hakika ni kinga kwake.”

Kwa sababu swawm inapunguza matamanio.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (17)
  • Imechapishwa: 01/12/2017