Swali: Niliamka siku moja wakati wa baridi kwa ajili ya kuswali fajr nikajikuta kuwa niliota. Nikioga basi swali ya fajr ingenipita ambapo nikawa nimetawadha na nikaenda kuswali. Je, kitendo hichi kinajuzu? Ni wajibu kwangu kurudi swalah hiyo au nifanye nini?

Jibu: Kitendo cha mtu huyu hakijuzu. Lililokuwa wajibu kwake ni kuoga. Kuoga ni kitu chepesi. Apashe maji, na huenda akawa na mashine ya kupashia maji, kisha aoge. Halafu aende na kuswali hata kama muda wa swalah utakuwa umeshatoka. Hata kama jua litachomoza katika hali hii ni mwenye kupewa udhuru.

Kuhusu atapochelea baridi na akawa hana kitu cha kupashia maji na badala yake akawa amefanya Tayammum na kuswali, swalah yake ni sahihi. Atapoweza kuyatumia maji atafanya hivo.

Anauliza kama swalah yake ile ni sahihi au si sahih? Tunamwambia lililo bora na salama zaidi ni yeye kuiswali tena swalah hiyo. Uhakika wa mambo ni kuwa aliiswali akiwa na janaba. Haijuzu kwake kwenda na kuswali msikitini ilihali yuko na janaba. Bali tunamwambia kuwa ni wajibu kwake kuoga hata kama mkusanyiko utampita.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (17)
  • Imechapishwa: 01/12/2017