Ikiwa huwezi kuzuia maovu kwa nguvu, kwa kuzungumza, basi chukia na uondoke hapo

Swali: Mimi ni kijana niliye na msimamo. Katika nyusiku hizi zilizobarikiwa wakati mwingine nakaa na baadhi ya vijana katika nyukumbi za starehe. Lakini wanaweza kuja wavuta sigara na wavuta bangi. Nifanye nini kutokana na hali hii?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule katika nyinyi mwenye kuona maovu, basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, afanye hivo kwa kuzungumza. Asipoweza, afanye hivo kwa mdomo wake.”

Akihudhuria katika kikao chenu mtu na akavuta sigara, kwanza unatakiwa kumnasihi. Akiacha basi hiyo ni kheri kwako na kwake. Asipoacha na wakati huohuo wewe ni muweza wa kumuondoa sehemu hiyo basi fanya hivo. Kwa sababu katika hali hii wewe ni muweza wa kuyaondoa maovu kwa kutumia mkono wako. Usipoweza, kwa mfano sehemu hiyo inamilikiwa na mwingine, basi wewe toka. Kwa sababu hukuweza kuzungumza wala hukuweza kwa kutumia mikono yako, kumebaki nini? Kutumia moyo. Moyo kamwe hauwezi kupinga kitu na ukabaki na yule mwenye kukifanya. Wewe toka. Kuna baadhi ya watu wanasema kuwa wanakaa nao na wakati huohuo wanachukia nyoyoni mwao. Tunasema: Ametakasika Allaah kutokaman na mapungufu. Huu ni mgongano. Lau kweli umechukia kwa moyo wako ni yupi aliyekulazimisha? Hakuna malazimisho yoyote. Kila mmoja ambaye anachukia kitu kwa moyo wake basi ni lazima ajitenge sehemu hiyo. Akidai kuwa yeye anachukia kwa moyo wake na wakati huohuo akabaki sehemu hiyo huyo ni mwongo. Tunamwambia iwapo kweli anachukia kwa moyo wake basi atoke. Vivyo hivyo inahusiana na mambo mengine yote yaliyoharamishwa. Ikiwa huwezi kuyaondosha basi toka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1604
  • Imechapishwa: 10/11/2018